Indirimbo ya 231 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwokozi alitoa damu kwa’jili ya waovu, msalabani alikufa kuniokoa mimi.
E’ Yesu, niokoe sana, nifunze kuamini! Na unilinde tena, Bwana, nisipotee kamwe!
2
Alijitwika dhambi zetu, huzuni na maradhi; neema kubwa, wema wingi, upendo wa ajabu!
3
Na hapo jua likafichwa, ikawa giza kuu; muumba alitufilia kutulipia deni.
4
Magoti yangu nayapiga msalabani pake, na kwa machozi natazama mateso yake huko.
5
Nitakurudishia nini, Mwokozi wangu mwema? E’ Bwana, nikutumikie maisha yangu yote!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 231 mu Nyimbo za wokovu