Indirimbo ya 104 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Lo! Horini Bethlehemu, ndani ‘nyumba ya ng’ombe, Bwana Yesu alilala usingizi wa kitoto. Nyota zilizo mbinguni kimya ziliangazia Bwana Yesu, mtulivu, juu ya ulalo wake.
2
Wachungaji wa kondoo walikuja kumwabudu, na majusi walifika wakamtolea tunu. Mungu mwenye macho yanayo tazama nchi yote, alivunja makusudi ya kuua ya adui.
3
Nakupenda, Bwana Yesu, kwani unaufaamu udhaifu wa mtoto, hali yake ya kitoto. Nawe sasa unaweza kunisaidia sana kila saa ya hatari, majaribu na mashaka.
4
Nakuomba, Bwana Yesu, unilinde njia yote, uwe mwenzi wangu mwema kila saa na dakika! Usichoke nami kamwe, nami sitaona hofu; Yesu unikumbatie siku zote na milele!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 104 mu Nyimbo za wokovu