Indirimbo ya 137 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nafurahi kwa sababu kati’ damu ya Yesu moyo umetakaswa, nimepata amani.
Haleluya! Haleluya! Mkombozi asifiwe! Haleluya! Haleluya! Haleluya! Amina!
2
Sina nguvu, ni dhaifu bila Yesu Mwokozi, ila kwa nguvu zake nasimama imara.
3
Moyo wangu, ufurahi, mimi mtu wa Yesu! Nampenda daima na kumtumikia.
4
Pendo kubwa la Mwokozi lanijaza rohoni. Nina raha kamili, moyo unastarehe.
5
Sifu Mungu, Baba yetu, Yesu Kristo Mwokozi, Roho Mtakatifu! Haleluya, Amina!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 137 mu Nyimbo za wokovu