Indirimbo ya 276 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Matendo ya Mungu yapita ‘fahamu, ni nani ayaona wazi? Lakini najua mapito ya Mungu kwa mimi yafaa halisi.
2
Njiani sijui maana ya yote, lakini nitayafaamu. Kwa nini kuzisumbukia kwa bure taabu na shida za mda?
3
‘ Bwana, unayo magari maelfu, na lenye linalonifaa, u’lichagulie mwenyewe, Bwanangu, nifike salama mbinguni!
4
Na kama Elia upesi kabisa nitakavyoacha dunia, uchungu na shida za huku ‘takwisha, milele nitashangilia.
5
Tutamsujudu Mwokozi daima, kuimba maelfu pamoja: E’ Mungu, u haki na mwenye neema katika shauri na tendo.
6
Halafu nangoja kwa uvumilivu kujua maana kwa wazi. Na matumaini ni yenye uzima: Urithi ninao mbinguni.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 276 mu Nyimbo za wokovu