Indirimbo ya 75 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Niliye msafiri, mgeni duniani; sioni kwangu hapa, ni huko ju’ mbinguni. Ninatamani nami kukaa siku zote pamoja naye Baba katika utukufu
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri wa binguni wapita yote huku.
2
Mwokozi yuko huko, rafiki yangu mwema, aliyenikomboa na ku’chukua dhambi. Na hata nikiona furaha siku zote ningali natamani makao ya mbinguni.
3
Na nikipewa huku vipawa vya thamani, na wakiimba nyimbo za kunifurahisha, rafiki wangu wote wakipendeza mimi, ningali natamani makao ya mbinguni.
4
Upesi nitaona kifiko cha mbinguni, Mwokozi wangu Yesu atanikaribisha; Na huko nitaona nilivyotumaini, kinubi nita’piga kumshukuru Yesu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 75 mu Nyimbo za wokovu