Indirimbo ya 191 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yapigwa hodi kwangu, mgeni a’fika, akiniomba: “Nifungulie! Umande umeshuka kichwani usiku, na nywele zangu zimelowa maji”.
2
A! Huyu si mgeni, ni Yesu Mwokozi, sauti yake nzuri na’jua. Ninamfungulia, naona ni Yesu; na siku hiyo sitaisahau.
3
Anong’oneza sasa rohoni: “U wangu”, karibu naye ninatulia. Ananitia nguvu, baraka ya mbingu; daima nitakaa kwake Yesu.
4
Ni kweli, mimi ni wa Mwokozi milele, amenitaja: “Ndugu, mpenzi”. Ananikarimia hazina za mbingu, ninaingoja siku ya arusi.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 191 mu Nyimbo za wokovu