Indirimbo ya 121 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yesu ni furaha yangu, amejaa pendo kweli. Anaweza kusimika kila mwenye udhaifu. Ananipa ujasiri, nguvu, raha na faraja. Hata nikionja kufa, Yesu ni mchunga wangu.
2
Nimefungwa na Mwokozi kwa kifungu cha upendo, hata kufa hakuwezi kunitenga naye Yesu. Mimi wake siku zote, ninataka kumtii. Kwa neema nimepona, nisitumikie dhambi.
3
Kwa mikono ya upendo ninakumbatiwa naye, sitaweza kutafsiri pendo lake kubwa kwangu. Napokea nguvu yake, yanijaza moyo wangu. Yesu ananiongoza katika safari yangu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 121 mu Nyimbo za wokovu