Indirimbo ya 275 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’ Mungu mwenye haki, uniongoze huku katika mambo yote yanayokupendeza! Nikiwa huku bila wewe, vitisho hofu na mashaka yananitia tetemeko mpaka kufa.
2
Ni heri siku zote kutegemea Yesu na kuenenda sawa katika nyayo zake, kwa kuwa yeye ni Mchunga anayeniongoza vema, nipate kuingia katika raha yake.
3
Safari yangu sasa yaelekea mbingu, Mwokozi yuko huko, lazima nifikeko na siku nitakapofika ‘tashangilia kwa furaha kuona yeye aliyeninunua kwake.
4
Ulimwenguni humu, matata na kuchoka. Nikihitaji kitu nafadhahika bure, lakini siku ile kuu nita’pomwona Mwokozi, natumaini sitakosa dhawabu yangu!
5
Mbinguni sitaona adui zangu tena. Hayatakuwa mambo yakupokonya pale. Sauti nitamtolea, kusema: Mungu, haleluya! Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 275 mu Nyimbo za wokovu