Indirimbo ya 33 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Huru kama ndege bustanini, sasa nafurahi kwa sababu Yesu ni rafiki yangu ‘kubwa; nina amani siku zote.
2
Aliniokoa na mashaka, alinipa tunu ya rehema. Mimi ni mtoto wa babangu, na nuru inang’aa sana.
3
Ninataka ku’shukuru Bwana, alitupa dhambi zangu mbali, na sitaziona tena kamwe, hazitanitawala tena.
4
Jua likifichwa kwa mawingu, kiti cha rehema ni karibu, hayo ndipo shida ziishapo, na roho yangu yatulia.
5
Radhi kama mwana kwa babake, kwa salama kama bandarini, Ninapumzika kwa Mwokozi, mbali na shida na huzuni.
6
Yesu yu karibu siku zote, achukua mimi na mzigo. Napokea kwa mkono wake neema na mateso pia.
7
Nilimpa Yesu moyo wangu, ninapenda kumtumikia; neno lake linapendwa nami, na nira yake ni laini.
8
Nafurahi sana kanisani kati ya watoto wa babangu, Roho ya neema ni karibu, kunanifurahisha sana.
9
Mimi ni mdogo duniani, tena msafiri na mgeni. Kwetu ni mbinguni huko juu; babangu ananiongoza.
10
Saa za mashaka zitakwisha, kuja kwake Yesu ni karibu. Nitaona raha kubwa sana katika nyumba ya babangu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 33 mu Nyimbo za wokovu