Indirimbo ya 6 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Twa’sifu Mungu kwa ajili ya damu takatifu, Inayotosha, kuondoa makosa yetu yote.
2
Wakristo wanakusanyika karibu ya kisima, hawapungukiwi kitu, wakaa kwa Mwokozi.
3
Tuimbe duniani pote juu ya pendo kubwa, kwa kuwa tumefunguliwa kisima cha Golgotha.
4
Kisima hicho, Yesu Kristo, na damu yake: damu yake. Wasumbukao wastarehe, waburudishwe hapa.
5
Na wenye dhambi wanaitwa kwa wingi wa rehema, na wakosaji na maskini wasaidiwa sana.
6
Tumeipata tunu kubwa, neema kwa neema, apokeaye fungu lake ni mtu wa uheri.
7
Haleluya! Tuna’himidi Mwenyezi na Mwanawe na Roho ‘takatifu pia. Haleluya! Amina.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 6 mu Nyimbo za wokovu