Indirimbo ya 17 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ukae nami, giza inafika! Usiniache, Mungu nakuomba! Unayejua udhaifu wangu, nategemea wewe, ‘kae nami!
2
Maisha yangu ni mafupi sana, uzuri wa dunia utakwisha. Kuna machozi, kufa huku chini, wewe Mwokozi wangu ‘kae nami!
3
Nakuitaji wewe siku zote, unaweza sana kunilinda. Wewe shujaa wakushinda wote. Katika hali zote ‘kae nami!
4
Unionyeshe msalaba wako, nione nuru yako kati’ giza! Na nikiishi au nitakufa. Wewe, Mwokozi wangu ‘kae nami!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 17 mu Nyimbo za wokovu