Indirimbo ya 69 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Je, tutaonana tena huko ng’ambo ya Yordani, na pamoja na wakristo ‘ona raha ya milele?
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!
2
Je, tutaonana tena, ba’da ya dhoruba zote huko katika bandari ya salama na amani?
3
Je, tutaonana tena kati’ mji wa dhahabu, Penye mto wa uzima nayo miti ya matunda?
4
Je, tutaonana tena na kusifu Mungu wetu miongoni mwa wakristo waimbao huko juu?
5
Tutaona na wapenzi waliotuacha huku? Je, tutawaona wote katika makao meme?
6
Tutaona Bwana Yesu katika kutano huko, tutakaribishwa naye katika karamu kuu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 69 mu Nyimbo za wokovu