Indirimbo ya 27 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Una uhodari leo wa kumfuata Yesu, hata ukichekwa sana na kuteswa duniani?
2
Una uhodari leo kuwa mtu wake Mungu? Ukiona haya sana, kisha utaona nini?
3
Mji unaonekana ukijengwa mlimani, hivyo na imani yetu inadhihirika sana.
4
Ukipenda Yesu na kuliko vitu vyote, unataka kumkiri, mbele ya wenzako huku.
5
Chuki au ‘pendeleo kwako kitu bure tena, watafuta siku zote sifa zake yesu Kristo.
6
Ujihoji nafsi yako ukitaka kuokoka! Uliekataa Mungu, tubu dhambi zako leo!
7
Umsihi masamaha, akuokoe ‘kati damu! Omba uhodari tena wa kumfuata Yesu!
8
Uchague Yesu leo, uwe mfuasi wake! Ukitwaa msalaba utaipokea taji!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 27 mu Nyimbo za wokovu