Indirimbo ya 76 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mgeni mimi, ninasafiri siku chache, siku chache huku chini. Msinipinge, niwafuate watakatifu walioshinda! Mgeni mimi, ninasafiri siku chache, siku chache huku chini.
2
Nashika njia, napiga mbio, sina budi kuukuza mwendo wangu. Na kwa mkono natwaa gongo, nazo silaha nimejivika. Nashika njia, napiga mbio, sina budi kuukuza mwendo wangu.
3
Ulimwenguni sipati raha, natamani ku’fikia mji mpya. Machozi, kufa, maombolezo sitayaona mbinguni tena. Ulimwenguni sipati raha, natamani ku’fikia mji mpya.
4
Mchunga mwema, ninakuomba, ‘tangulie, niongoze njia yote, kwa kuwa giza na dhambi tena zaniwekea mitego mingi! Mchunga mwema, ninakuomba, ‘tangulie, niongoze njia yote!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 76 mu Nyimbo za wokovu