Indirimbo ya 34 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Kwa pendo lake kubwa alitafuta mimi, na alinichukua begani mazizini na nyimbo zao malaika zikajaza mbingu pia.
Alinitafuta, akaniokoa, akaniondoa matopeni, akanichukua mazizini.
2
Mchunga mwema Yesu aliniponya roho, na akaniambia: «Mtoto upendwaye». Sauti yake ya upendo ikaufariji moyo.
3
Ninakumbuka jinsi alivyotoka damu, na taji ya miiba, mateso ya mauti. Na penye msalaba wake ninashukuru Bwana Yesu.
4
Namfuata yeye katika nuru yake, waridi za ahadi zapamba njia yangu. Milele nitaendelea kusifu Yesu kwa furaha.
5
Na saa zinapita, nangoja asubuhi utakaponiita, niende kwako juu. Nitasimama kwa amani mbinguni mbele yako, Yesu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 34 mu Nyimbo za wokovu