Indirimbo ya 146 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Karibu na wenzangu nilipotea njia, rohoni mwangu njaa, na sikuona raha, lakini sasa Yesu ni Mchungaji wangu, naandamana naye siku zote.
2
Katika shamba lake nimefuata Yesu, ninapajua anapolisha kundi lake. Na penye maji hai napunzika sana, naona raha hapo siku zote.
3
Lakini mchungaji apita vitu vyote, uzima aliweka kwa ‘jili ya kondoo. Nikumbukapo Yesu, sioni tena kitu cha kupendeza ila yeye, Bwana.
4
Naimba kwa furaha rohoni mwangu hivi: « Upendo wako, Yesu, ninausifu sana!» Na jina lake Yesu ni kama manukato; ananilinda vema siku zote.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 146 mu Nyimbo za wokovu