Indirimbo ya 118 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ni Mwokozi mzuri ninaye, alikufa kunikomboa. Alitoa uzima wake kwa ajili ya watu wote
Alikufa msalabani, alikufa msalabani. Kwa ajili ya dhambi zangu zote alikufa msalabani.
2
Aliacha makao juu, akafika ulimwenguni; aliteswa kwa’jili yangu na kunifungulia mbingu.
3
Dhambi zangu ali’chukua, kujitwika hukumu yangu, na alijeruhiwa ili aniponye na ‘nipa raha.
4
Bwana Yesu alifufuka, akarudi mbinguni kwake; na yuaja upesi tena achukue walio wake.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 118 mu Nyimbo za wokovu