Indirimbo ya 232 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nilipofika kwa Bwana Yesu, nikapaaza sauti yangu: “Yesu Mwokozi, unirehemu!” Akaniokoa.
:/: Yesu asifiwe! :/: Alisikia kilio changu, Yesu asifiwe!
2
Nilipofika kwa Bwana Yesu, nikamsihi Mwokozi wangu: “Unitakase, nifanye safi!” Akanisikia.
:/: Yesu asifiwe.:/: Alisikia maombi yangu, Yesu asifiwe!
3
Ona kisima cha msalaba, leo kingali chabubujika kuniokoa na kusafisha! Yesu asifiwe!
:/: Yesu asifiwe:/: Aniokoa, anisafisha, Yesu asifiwe!
4
Njoo kwa Yesu, kisima hicho, unywe, uoshwe katika maji! Kiu yapoa, na watakaswa, Yesu asifiwe.
:/: Yesu asifiwe! :/: Kiu yapoa, na watakaswa, Yesu asifiwe!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 232 mu Nyimbo za wokovu