Indirimbo ya 129 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ninataka kumsifu Yesu Kristo aliyeondoa dhambi zangu zote. Twende sote sasa tumsifu Yeye, na pendo kubwa la Mwokozi!
Haleluya! Yu Mfalme ‘kuu! Haleluya! Asifiwe! Alinisamehe dhambi zote; alinilinda kwa salama!
2
Na baraka yake anaimimina, kama mvua inyeshavyo juu yangu. Nastarehe mikononi mwake Yesu, rehema yake inatosha.
3
Siku moja nitamwona Yesu Kristo kati’ nchi nzuri sana ya furaha, macho yangu yatamtazama yeye, kuona sura ya Mfalme.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 129 mu Nyimbo za wokovu