Indirimbo ya 29 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Univute, Yesu, nifuate nyayo zako, ‘kiwa kwa rafiki au katika wageni, na mahali pa furaha au sikitiko; sina budi kumkaribia Yesu.
Nimfuate, nimkaribie, siku zote na popote nimwandame Yesu! Nimfuate, nimkaribie, Yesu mbele, nami nyuma, hata mwisho!
2
Juu ya milima nitasikiliza Yesu, hata mabondeni nitaandamana naye. Jua, giza, afya, ‘gonjwa, utulivu, vita, kati’ hayo yote Yesu yu karibu.
3
Nikiteka maji, au nikilima shamba, nikika’ nyumbani au ‘kiwa safarini, hata huko soko neno moja ni halisi: Sina budi kumkaribia Yesu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 29 mu Nyimbo za wokovu