Indirimbo ya 319 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nafurahia wokovu niliopata kwa Yesu, nitasifu Mungu wangu daima huko mbinguni. Wokovu niliopewa, na unanirusha juu, kw’ajili ya shangwe kubwa, inayoimba rohoni.
2
Silinganishe wokovu wangu na kitu kingine. Kwani vyote vinakosa, bei ya wokovu wangu. Mwokozi alinifia, alinilipia damu, nayo ni ya bei ghali, safi ya Mwana wa Mungu.
3
Ninaupenda wokovu, wanitosha kwa matata, kwani Bwana wa wokovu, hakufuata makelele. Aliwaponya wagonjwa, na alifufua wafu, akahubiri injili, alituonyesha njia.
4
Ninakusifu Mwokozi, kwani umeniokoa, umenitosha kwa giza, na sasa niko nuruni. Mwenye upendo ni wewe, neema yake ni kubwa, ulinitosha kabisa, katitka pori na giza.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 319 mu Nyimbo za wokovu