Indirimbo ya 10 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Damu yako yenye baraka inayo tuosha makosa, ilimwagwa msalabani, Bwana Yesu, ulipokufa. Nastahili ‘pata hukumu, na siwezi mimi kujiosha. Unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa.
Safi, safi kweli, safi, safi kweli! Unioshe katika damu, nipate kuwa safi kabisa!
2
Yesu, ulivikwa miiba, kuangikwa juu ya mti. Ulivumilia mateso, maumivu na majeraha. Ninataka kijito hicho, n’ende na nikasafishwe sana! Unioshe katika damu, nipate kuwa safi kabisa.
3
Baba, kweli nina makosa, moyo wangu wa udhaiffu; mimi mwenye dhambi rohoni nitaona wapi Mwokozi? Yesu, kwako msalabani naja, ninakuamini sasa.. Unioshe katika damu,, nipate kuwa safi kabisa.
4
Bwana,, nimefika karibu,, unilinde kwako milele! Ufungue kila kikamba, unijaze moyo mwenyewe. Na karibu ya msalaba nitakaa hata kufa kwangu. Unioshe katika damu,, nipate kuwa safi kabisa



Uri kuririmba: Indirimbo ya 10 mu Nyimbo za wokovu