Indirimbo ya 56 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yesu, ninakutolea vyote ninakuwa navyo, nikupende, nifuate wewe siku zote hapa!
Ninakupa vyote, ninakupa vyote, Bwana Yesu upendwaye, ninakupa vyote.
2
Miguuni pako, Yesu, ninakusujudu sasa. Ninakutolea vyote: roho, moyo na maungo.
3
Najitoa kwako, Yesu, nafsi yote iwe yako! Bwana Yesu, nakusihi: Niwashie moto wako!
4
Yesu, ninakupa vyote, unijaze Roho yako! Nisikie moto wako ukiwaka ndani yangu!
5
Vyote ninakupa, Bwana, viwe mali yako kweli! Na fahari ya dunia naiona ni ya bure.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 56 mu Nyimbo za wokovu