Indirimbo ya 81 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Alipokufa Yesu ju’ ya msalaba wake akaishinda dhambi na uwezo wa shetani. Aliniweka huru, niwe mbali na hatia; na tena atanichukua kwake.
Mbinguni niendako haitakuwa dhambi, ni nchi nzuri ya salama mno. Na Bwana, Mungu wetu, atatuangazia; tukusanyane sisi sote humo!
2
Ninafuata njia ya Mwokozi wangu sasa, aniongoza vema, anafuta kila chozi. Ananilinda katika hatari za njiani, karibu naye vita yatulia.
3
Mbinguni nchi yangu, na bendera ni upendo, na Roho arabuni ya urithi wangu huko; na neno lake ni chakula changu safarini; neema inanipeleka kwake.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 81 mu Nyimbo za wokovu