Indirimbo ya 247 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Napenda sana kumshukuru Mwokozi wangu kwa nia huru; kwa wimbo wangu nashuhudia upedo wake na damu pia.
2
Nikishukuru mateso yake msalabani na kufa kwake, nataka katika wimbo wangu kumtolea shukrani yangu.
3
Naimba sasa, nina faraja, katika Yesu nina faraja. Ni mambo tunayofunuliwa, kwa wenye dhambi yamefichwa.
4
Kwa neno lake ananiambia kwamba ananihurumia, na ukombozi ninao sasa kwa damu iliyonitakasa.
5
Na msione ajabu sana ya kuwa namshukuru Bwana! Ninamwimbia kidogo sasa, ‘taendelea mbinguni hasa.
6
Anipa vyote kwa pendo lake, urithi wangu wachungwa kwake hata wakati wakuhamia mbinguni, na nitashangilia.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 247 mu Nyimbo za wokovu