Indirimbo ya 16 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yo yote uonayo huku katika mwendo wako, yafaa ku’mwambia Yesu, atakusaidia.
Kwa kuwa kila aombaye Mwokozi neema yake, ataokoka na hatia, na atasifu Yesu.
2
Ukichukiwa na rafiki na ukijaribiwa, Mwokozi yu karibu sana, maombi asikia.
3
Ukiwa mwana mpotevu, na mbali na babako, amani una’kosa sasa, urudi kwake Yesu!
4
Ukiwa na makosa mengi, na roho yako ngumu, neema yake yakutosha, utubu dhambi zako!
5
Ikiwa nguvu mara nyingi kuomba kwa bidii, uombe Baba, kama mwana, akusikia kweli!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 16 mu Nyimbo za wokovu