Indirimbo ya 157 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Haidhuru kwangu huku chini utajiri au umaskini, ila Bwana Yesu awe nami; ninatunzwa naye siku zote.
2
Haidhuru kama ninakuta shida nyingi katika safari, ila Mchungaji wangu mwema anilide na kuniongoza.
3
Haidhuru kama tunakaa katika baridi au hari, kwa sababu ukombozi wetu unakaribia. Haleluya!
4
Haidhuru kama sitapata utukufu na heshima huku; nikifanywa kama takataka, yanipasa kupendeza Bwana!
5
Haidhuru kama njia yangu inanichokesha mara nyingi, basi, nisigombane na ndugu, na pamoja tutashangilia!
6
Haidhuru kama tukiona sisi si wakubwa huku chini. Tuwe watumishi wake wema, na tutaingia kwake Bwana!
7
Haidhuru kama twasafiri katika dhoruba ya bahari, kwani Yesu ni nahodha wetu, atatufikisha bandarini.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 157 mu Nyimbo za wokovu