Indirimbo ya 110 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwamba uliopasuka, ndani yako nijifiche! Maji yale, damu ile itokayo mbavu zako, iwe dawa ya kuponya roho yangu na ubaya!
2
Kazi za mikono yangu, haziwezi kukomboa. Hata ningelia sana na kutenda kazi nyingi, singeweza kuokoka, peke yako u Mwokozi.
3
Ndani yangu sina kitu, naushika msalaba. Uchi mimi, univike! Sina nguvu, ‘nichukue! Ni mchafu, unioshe! Wewe u Mwokozi wangu.
4
Kwa maisha yangu yote hata nitatoa roho, hata saa ya kuitwa mbele ya Mfalme wangu, mwamba uliopasuka, nijifiche ndani yako!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 110 mu Nyimbo za wokovu