Indirimbo ya 101 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’ mlinzi, twauliza: Yesu atakuja lini? Asubuhi ya sayuni ni karibu? Tuambie! Msafiri, yainue macho yako, angalia! Asubuhi ni karibu, usimame, usimame!
2
Siku heri ya sabato ya milele ni karibu, na dalili yake Yesu hapo itaonekana. Na rohoni tunaona nchi nzuri ya ahadi. Asubuhi ni karibu, na ahadi zatimia.
3
Katika Yerusalemu, mji mpya wa mbinguni, Yesu atatumiliki kwa upendo na amani. Baragumu italia, nasi tutaisikia. Yesu ni karibu sana kutukaribisha kwake.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 101 mu Nyimbo za wokovu