Indirimbo ya 88 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mponyi apitaye wote amefika hapa. Awaponyesha watu moyo. Yesu wa upendo.
Jina linalopita yote juu na chini pote pia, jina kubwa, jina jema: Yesu wa upendo.
2
Awasamehe watu dhambi wakizitubia, awapokea kwa neema, waipate afya.
3
Tukiwa na masikitiko, Yesu afariji. Akitubarikia sana, woga waondoka.
4
Watoto walipenda sana jina lake Yesu, liwalindalo na mabaya, wakijaribiwa.
5
Shetani aogopa sana jina lake Yesu. Katika vita ju’ ya dhambi latutia nguvu.
6
Mbinguni tena kwa furaha tutamwona Yesu. Tutasahau shida zote, tutamshukuru.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 88 mu Nyimbo za wokovu