Indirimbo ya 233 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tazama Mwokozi aliyekufilia ili wewe upate uzima! Tazama, kwa pendo atakusaidia, usidumu dhambini daima!
Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!
2
Mwokozi alisulibiwa ju’ ya mti ili sisi tupate wokovu. Alitukomboa kwa damu yake safi, kwate yeye twapata wongofu.
3
Hakuna majuto yaweza’ kutuponya, ila damu ya Yesu Masiya. Ufike kwa Yesu apate kukuonya jinsi yaondokavyo hatia!
4
Rafiki, waitwa na Mungu kwa wokovu, anataka ufike upesi. Kwa nini kukawa, ufike bila hofu, uondoke katika hatari!
5
Ufike, pokea uzima wa milele, Bwana Yesu ali’tuletea! Karama ya mbingu ni tumaini letu, ipokee na hutapotea!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 233 mu Nyimbo za wokovu