Indirimbo ya 58 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Unipe raha tele kama mto, nipite jangwa huku kwa furaha; unipe imani tena, Yesu, ningoje siku yako kwa bidii!
2
Kwa siku chache ninaona shida, dhoruba zinanisumbua huku. Napanda mbegu zangu nikilia, lakini nitavuna kwa furaha.
3
Kwa siku chache ninaburudishwa mtoni penye njia yangu huku, lakini siku kubwa itafika, nita’inywea chemchemi yake.
4
Kwa siku chache naitunza taa, nadumu kwa kuomba na kungoja. Na siku za uchungu ziishapo, nitamkuta Yesu huko juu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 58 mu Nyimbo za wokovu