Indirimbo ya 294 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya hapo kale! :/: Uwashe moto wako ndani yetu, tusiwe watu wa uvuguvugu! :/:
2
Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya siku ile. :/: Mtume Petro alipohubiri katika nyumba yake Kornelio! :/:
3
Utume Roho yako juu yetu, utupe nasi Pentekoste yetu! :/: Maelfu wenye dhambi waokoke, na neno lako lienee pote!:/:
4
Utume Roho yako juu yetu! Mikono yako uinyoshe sasa,:/: ishara za ajabu zifanyike, wagonjwa uwaponye kati yetu! :/:
5
Uwaamshe waliosinzia, waliochoka huku safarini! :/: E’ Bwana utujie kama kale ulivyowabariki watu wako! :/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 294 mu Nyimbo za wokovu