Indirimbo ya 128 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nina rafiki mwema, naye alinifilia; alinivuta kwake na amenifanya mpya. Ni mali yake Yesu tu, ninaongozwa naye, alikomboa mimi kwa agano la upendo.
2
Nina rafiki mwema, na aliondoa dhambi, aliniweka huru na kunipa Roho yake. Na vitu vyote ninavyo ninavitoa kwake, maisha yangu ni yake, yaimba sifa zake.
3
Nina rafiki mwema na anayeweza yote, pamoja naye Yesu tu nashinda majaribu, atanitwaa kwake ju’ mbinguni kwa furaha; Nitastarehe katika makao ya milele.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 128 mu Nyimbo za wokovu