Indirimbo ya 65 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Huko ju’ ya nyota zote kuna nchi yenye mema, Mji wake ni Yerusalemu; Dhambi haitakuwamo, wala kufa na huzuni, Kwake yesu nitapata kao.
Sikitiko na machozi hayatakuwako huko, Wala giza au vita ya dunia. Huko hatutayaona mambo ya kutuumiza. U Yerusalemu ‘takatifu!
2
Nifikapo mji huo nitaona Yesu kwanza, aliyechukua dhambi zangu. Nitaona uso wake, nitamshukuru yeye aliyeniweka huru kweli.
3
Huko nitaona tena jeshi la walioshinda kwa imani huku duniani, na pamoja nao wote nita’sifu Mungu sana juu ya neema yake kubwa.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 65 mu Nyimbo za wokovu