Indirimbo ya 52 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Kwa salama Baba Mungu awalinda watu wake, hata nyota za mbinguni si salama kama wao.
2
Mungu awalinda hivyo katika upendo wake. Wanakumbatiwa naye, wanarehemiwa sana.
3
Hawavutwi toka kwake kwa furaha wala shida. Yeye ni rafiki ‘kubwa wa walio watu wake.
4
Wanalishwa, wanavikwa, wanafarijiwa naye. Hata nywele za kichwani zimehesabiwa zote.
5
Enyi kundi lake dogo, Mungu atawahifadhi! Na adui watashindwa kwa uwezo wake ‘kubwa.
6
Akitoa, akiwapa, baba yetu hageuki. Na mapenzi yake ndiyo: Wana wapatishwe wema.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 52 mu Nyimbo za wokovu