Indirimbo ya 274 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ninafurahia kisima daima, kisima cha damu ya Yesu. Katika upendo nalindwa salama, nasifu Mwokozi mpendwa.
Kisima cha maji kinabubujika, kinaniletea uzima. Na kando ya maji ninaburudika, ninashangilia daima.
2
Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi kwa maji ya ‘hai. Yananilietea kupita kipimo uzima na shangwe rohoni.
3
Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi katika uheri. Ufike upesi ulie na kiu, kisima kinabubujika!
4
Nakaa karibu ya kisima hiki, naona furaha na raha. Nakando ya maji nafasi kwa wote, waweza kupona kabisa.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 274 mu Nyimbo za wokovu