Indirimbo ya 98 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Siku moja tutaona utukufu wake Yesu, kama nuru ya umeme atakavyoonekana.
Uhubiri neno lake, kwa bidi’ mahali pote! Siku ni karibu sana; Bwana Yesu atakuja.
2
Tangu kale tumengoja siku ya uhuru wetu. Hata nguvu ya mauti itaisha siku ile.
3
Heri gani ya wakristo kumlaki Bwana yesu! Watavikwa nguo safi huko juu kwa Mwokozi.
4
Pasha hi’habari njema, na wagonjwa uwaponye! Uokowe wapotevu! Wende mbio, usikawie!
5
Kwa dalili tunaona kwamba Yesu yu karibu, na Mfale atakuja ‘tupeleka kwake juu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 98 mu Nyimbo za wokovu