Indirimbo ya 243 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ukichoka kwa safari ngumu, sema na Yesu, sema na Yesu! Waogopa kwamba hutadumu, sema na Yesu daima!
Sema na Yesu, sema na Yesu, yeye rafiki amini! Akupenda kwa upendo bora. Sema na Yesu kwa yakini!
2
Ukilia chozi ya majuto, sema na Yesu, sema na Yesu! Ukiteswa ju’ ya dhambi nzito, sema na Yesu daima!
3
Je, wahofu jua likifichwa? Sema na Yesu, sema na Yesu! Kwa taabu ukihuzunishwa, sema na Yesu daima!
4
Ukisumbukia kufa kwako, sema na Yesu, sema na Yesu! Ukiteswa kwa maisha yako, sema na Yesu daima!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 243 mu Nyimbo za wokovu