Indirimbo ya 40 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ameniwaka huru kweli, naimba sasa: Haleluya! Kwa msalaba nimepata kutoka katika utumwa.
Nimeokoka, nafurahi! Na dhambi zangu zimetoka. Nataka kumtumikia Mwokozi wangu siku zote.
2
Zamani nilifungwa sana kwa minyororo ya shetani, nikamwendea Bwana Yesu, akaniweka huru kweli.
3
Neema kubwa nilipata kuacha njia ya mauti, na nguvu ya wokovu huo yanichukua siku zote.
4
Na siku moja nitafika mbinguni kwake Mungu wangu. Milele nitamhimidi na kumwimbia kwa shukrani.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 40 mu Nyimbo za wokovu