Indirimbo ya 169 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Askari wa imani sisi, kwa shangwe tunaendelea, hata vita ‘kiwa kali tuna nguvu na ‘hodari. Tuna upanga wa imani, ni neno lake Mungu wetu; na kwa jina lake Yesu tunashangilia sasa.
Mbio tutaacha huku, vita ikiisha. Tutaingiamo mbingu ku starehe humo. Wao washindao huku, watapewa taji kwa mkono wa Mwokozi, anayewapenda.
2
Tuvae kila mtu sasa silaha zote zake Mungu. Na mishale ya shetani ‘tazimika mbele yetu. Tukimtii Bwana Yesu, twaendelea kwa ‘hodari, na kwa nguvu za ahadi tutakuwa washindaji.
3
Na ukipungukiwa nguvu, katika vita ukishindwa, Yesu atakutilia nguvu mpya ya kushinda. Kwa nyimbo za kushangilia, utahimili shida zote, na kupata kuokoa wenye dhambi na makosa.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 169 mu Nyimbo za wokovu