Indirimbo ya 196 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Usiyefanya bidii kabisa, hutaingia mbinguni. Uikinge roho kwa neno la Mungu, usipotee milele! Njia ni nyembamba na mlango ‘dogo, ujitahidishe kuingia humo! Ukubali leo wokovu wa Mungu ili ufike mbinguni!
2
Vizuio vingi katika safari, mwovu anakujaribu. Uvishinde vyote vinavyozuia, vyote katika dunia! Usimfuate kila aitaye, ungeweza kupoteza roho yako! Bwana Yesu anakupenda daima; ujitahidi kabisa!
3
Pasipo imani huwezi kufika hata bandari salama wala kuingia katika uzima; hilo ni neno la Mungu. Kwa imani tupu utaokolewa, usikie sasa neno la wokovu! Tubu dhambi zako, amini Mwokozi; hiyo ni njia, hakika.
4
Mungu anaita, wo wote wafike, waupokee uzima! Atakupa nawe hazina ya mbingu, ukitafuta kwa kweli. Mungu Baba anapenda roho yako, Yesu anataka kuokoa wewe, Roho ‘takatifu anakuamsha. Ukiitika u heri!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 196 mu Nyimbo za wokovu