Indirimbo ya 49 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Njia yote naongozwa kwa mkono wa Mwokozi, ninapo wema wake, sina shaka, hofu tena. Nina raha ya mbinguni, ninakaa kwa salama. :/: Na katika mambo yote ananitendea mema. :/:
2
Njia yote naongozwa, namtegemea Yesu. Anilinda jaribuni, anitia nguvu pia. Nikiona kiu hapa, nikichoka safarini,:/: Mwamba uliopoasuka unabubujika maji. :/:
3
Njia yote naongozwa kwa mkono wake bora, atanituliza tena kwa babake huko juu. Miguuni pake Yesu ninataka kusujudu,:/: Nakusifu yeye, kwani aliniongoza huku. :/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 49 mu Nyimbo za wokovu