Indirimbo ya 134 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Watu wa Mungu, mshangilieni kabisa, na mwimbieni Mfalme wa mbingu na nchi! Mungu yu nasi kwa pendo kubwa, kamili ili tupate wokovu.
2
Ona ajabu! Mwokozi aliyejidhili! Pendo kamili na neema nyingi ya Mungu: Alizaliwa, akawa mwana Adamu, atukomboe na dhambi!
3
Sisi wakristo tumwimbie tena pamoja Yesu Mwokozi aliye dhabihu ya kweli! Na atukuzwe hapa na huko mbinguni, kwani alitufilia!
4
Yesu Mfalme, kwa pendo uliniokoa, nikufuate, nikutumikie daima! Huko mbinguni nitakusifu milele katika watakatifu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 134 mu Nyimbo za wokovu