Indirimbo ya 355 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Kwa kilima cha mbali, kulikuwa na mti, mfano wa shida na haya. Mti ule ni hapo Yesu akawa kweli dhabihu na dhambi na deni.
:/: Naupenda msalaba ule nguvu zake zanipa kushinda, Msalaba naukumbatia hata nitakapo pata taji :/:
2
Msalaba wa kale, umenivuta kwake, Ujapo tupiwa zarau. Mwana-kondoo safi alikufa Golgotha mabegani aliuchukua.
3
Msalaba wa kale wenye damu ya Yesu, uzuri ajabu unao. Yesu Mwana wa Mungu, aliteswa akafa na wokovu alitupatia.
4
Msalaba wa kale, naupenda daima, Ingawa dhihaka na bezo. Hata ananiita, kwenda kwake mbinguni, kushiriki utukufu wake.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 355 mu Nyimbo za wokovu