Indirimbo ya 148 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nguvu ile ilishuka ju’ ya wanafunzi wote mjini mwa Yerusalem’ siku ya Pentekoste, lo! Nguvu hiyo ya Mwokozi ni sawa leo; shukuru Mungu!
:/: Karama, karama, karama yake Mungu ni sawa hata leo, ni sawa hata leo!:/:
2
Yesu aliwapa ahadi: «Mtapokea nguvu». Na Roho akashuka na wakamsifu Mungu. Walio wenye udhaifu, wakahubiri kwa uthabiti.
3
Roho yule aingiapo anatutia nguvu, tupate kwa imani ku’ kushinda yule mwovu. Kwa moyo wenye moto safi tuite watu kwa Mkombozi!
4
Uingie sasa rohoni, uwashe moto wako, tupate kusimama kwa usafi siku zote! Ufike sasa kama mbele wakati huo wa Pentecoste!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 148 mu Nyimbo za wokovu