Indirimbo ya 322 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nashika njia ya kwenda mbingu, mimi msafiri duniani, naishi kwa taabu na mateso mengi. Bali nakaza mwendo nifike mbingu.
2
Ijapo shida zanizunguuka, mimi msafiri njia, nashika njia nifike mbingu; nitarithi pamoja na Yesu, nitarithi pamoja na Yesu. :/:
3
Wenzangu wote wananigombeza na marafiki wananicheka. Nasumbuliwa hata na wanangu, natazama Yesu rafiki Mwema.
4
Ninachofanya maishani mwangu, nimpendeze Mungu aliye Mwema. Nijapoteswa, ninatumaini kuingia mbingu, ni nchi ya raha.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 322 mu Nyimbo za wokovu