Indirimbo ya 283 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nimeyasikia mengi aliyoyafanya Yesu katika maisha yake huku chini: Pote alitenda mema, alisaidia wote. Kwa furaha ninaimba: “Yesu yeye yule leo!”
Yesu Kristo yeye yule jana, leo, siku zote. Hutafuta wapotevu, huokoa na waovu. Mwokozi wetu yeye yule!
2
Na kipofu yule, jina lake ndilo Bartimayo, aliposikia Yesu yu karibu, kwa imani akaomba, akapona kwa neema. Nafurahi kwa kuimba: “Yesu yeye yule leo!”
3
Watu wote wenye dhambi na wagonjwa na maskini wanaitwa kwake Yesu kwa rehema. Uiguse nguo yake, sawa mwanamke yule, utapewa nguvu yake, kwani Yesu yeye yule!
4
Nimeyasikia tena jinsi alivyoombea maadui wake ju’ ya msalaba. Aliteswa kwa miiba, aliona maumivu. Ninaimba kwa furaha: “Yesu yeye yule leo!”



Uri kuririmba: Indirimbo ya 283 mu Nyimbo za wokovu