Indirimbo ya 268 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’ Yesu, ingia rohoni kabisa, uniweke huru nakunitakasa, nipate kushirikiana na wewe katika mateso na raha daima!
:/: E’ Bwana, nijaze upendo wa mbingu nao uthabiti, niwe mshindaji! :/:
2
Siombi ufalme, siombi heshima, naomba kupewa neema daima, nijue ukweli wa neno la Mungu: Mtoe miili na iwe dhabihu!
3
Ingia rohoni, unichungulie, na katika yote unisaidie, nipate kabisa kusudi na nia kujitoa kwako, kukutumikia!
4
Hakuna la huku litanizuia nisifananishwe na Yesu Masiya. Nitumainije kufika mbinguni nisiposhiriki Mwokozi mpendwa!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 268 mu Nyimbo za wokovu