Indirimbo ya 312 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Zaburi 117:1-2. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, enyi watu wote mhimidi. Maana fadhili zake, kwetu sisi ni kuu, na uaminifu wa Bwana ni wa milele.
Zaburi 118: 1-7,2. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Kwa kuwa fadhili zake ni za milele. Israeli na aseme sasa, ya kwamba fadhili zake, ya kwamba fadhili zake ni za milele.
2
Mlango wa Haruni na waseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele. Wamchao Bwana na waseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3
Katika shida yangu nalimwita Bwana. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; mwanadamu atanitenda nini? Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, msaidizi wangu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 312 mu Nyimbo za wokovu